Habari

Serikali yatoa onyo kali kwa magazeti ya Mwananchi na The Citizen ‘tunawapa nafasi ya mwisho wajitafakari’

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa onyo kwa magazeti ya Mwananchi na The Citizen kwa kuyataka yajitafakari kwa kile ilichooeleza kuwa wameandika habari za “uongo wa karne”.

Image result for hassani abbasi magazeti mwananchi
Dkt. Hassan Abbasi

Akitoa onyo hilo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi Hassani kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema kuwa magazeti hayo kwenye matoleo yake ya mtandaoni yalichapisha habari za uongo, huku wakitumia takwimu zisizo rasmi.

Ufafanuzi: Jana magazeti ya the Citizen na Mwananchi matoleo ya mitandaoni yalibeba habari iliyodai wahisani wametoa 6.7% tu kwenye bajeti. Habari hii ni uongo wa karne. Takwimu zilizowekwa hata kwenye viambatishi vya hotuba ya Waziri zinaonesha imetolewa 69% kufikia Jan., 2019.

Kwa makosa haya yanayojirudiarudia na yenye nia ovu (kwa kuwa hawakutaka hata ufafanuzi wa Serikali au nyaraka), Serikali inayapa nafasi ya mwisho magazeti ya Mwananchi na the Citizen kujitafakari tena kama yana sababu, nia na dhamira ya kuendelea na kazi hii.

Dkt. H.A.

Onyo hilo linakuja ikiwa ni wiki moja imepita, tangu gazeti la The Citizen kurejea mtaani, baada ya kufungiwa kwa wiki moja na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents