Habari

Serikali yatoa tamko kufuatia tukio la Mwalimu kumchapa mwanafunzi viboko hadi kumuua ‘hajatumwa, ile bahati mbaya’

Serikali imetoa tamko lake kwa mara ya kwanza tangu litokee tukio la mwalimu wa shule ya msingi ya Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kumchapa fimbo mwanafunzi wa darasa la 5 aliyejulikana kwa jina la Sperius Eradius (13) kwa tuhuma za kuibiwa mkoba.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako

Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akiongea na Waandishi wa Habari leo Jumatano Agosti 29, 2018, amesema kuwa tukio hilo lilikuwa ni la bahati mbaya na tayari hatua za kisheria zimechukuliwa.

Muwe na amanai na utulivu katika kipindi hiki ambacho serikali inafanya kazi yake nadhani mmemsikia kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ameongea vizuri kabisa na hiyo ndio tamko la serikali. Yule hajatumwa na serikali kufanya yale aliyoyafanya. Na niwahakikishie wananchi kuwa shule ni sehemu salama kwa hiyo asitokee mtu ambaye akafanya vitendo ambavyo vitamfanya mzazi au watotot waone shule kuwa sio sehemu salama,“amesema Prof. Ndalichako na kusisitiza kuwa tukio hilo lilikuwa ni bahati mbaya.

Kwa hiyo ni bahati mbaya ambayo imetokea, lakini bahati mbaya hiyo kwa namna yoyote ile isije ikatafsiriwa kama ndio sasa shule sio sehemu salama, na yoyote yule anayehatarisha usalama shuleni serikali itamshughulikia kwa nguvu zote. Kwa sababu serikali inaamini elimu ndio nyenzo muhimu ya maendeleo ndio maana serikali kwa mwezi inatoa bilioni 20 kugharamia elimu.“amemaliza Waziri Ndalichako.

SOMA KWA UFUPI KUHUSU TUKIO LA MWALIMU HUYO LILILOPELEKEA  KUMCHAPA MWANAFUNZI HUYO HADI KIFO:

Mwanafunzi wa darasa la 5 katika Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius(13) amefariki dunia akidaiwa kupigwa na mwalimu wake kwa kutuhumiwa kuiba pochi ya mwalimu

Baadhi ya Wanafunzi walioshuhudia tukio hilo lililotokea jana (Juzi Jumatatu) wamesema mwanafunzi huyo alikwenda kumpokea mizigo mwalimu wake aliyefika shuleni hapo kwa usafiri wa bodaboda

Alipoingia ofisini Mwalimu huyo alianza kulalamika kutoiona pochi yake ndipo Sperius alipoitwa na kuhojiwa lakini akakana kuichukua hali iliyosababisha kuanza kupigwa akitakiwa kuirejesha

Aidha, waliongeza kuwa baadaye walitakiwa kuitafuta pochi hiyo hadi chooni, lakini hawakuiona huku mwanafunzi huyo akiendelea kuadhibiwa

Hata hivyo, dereva bodaboda alifika shuleni hapo akimtafuta mwalimu aliyepoteza pochi na kumkabidhi pochi aliyokuwa ameisahau kwenye pikipiki yake

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoani humo, Dkt. John Mwombeki, alikiri kupokea mwili wa mtoto huyo majira ya saa mbili asubuhi ukionekana kuwa na majeraha.

Related Articles

27 Comments

  1. Haya mambo atakuja uliwa mwalimu na mseme hivyo hivyo bahati mbaya msitutanie na uongozi wenu kwanza waziri ndio karuhusu adhabu ya viboko Leo anaongea urojo wake hapa eti bahati mbaya kuua

  2. Kitafiti, ni vigumu kwa mtoto kuuawa kwa kuchapwa fimbo matakoni. Labda iwe mchapwa ana matatizo ya kiafya. Fikiria ikiwa huyo mtoto kachapwa tu matakoni akafa vipi kuhusu angepigwa ngumi ya usoni au kichwani na Mwanafunzi mwenzake? Hapa mimi namlaumu wazazi wa huyo mtoto. Huenda walificha au hawakujua matatizo ya kiafya ya mtoto. Wazazi tunashauriwa kuwafanyia checkup watoto kila mwaka ili kubaini matatizo ya kiafya ya watoto wetu ili kuweza kuweka makanizimu bora nyumbani na shuleni jinsi ya kumwangalia mtoto na kumpatia adhabu sahihi kulingana na afya ya mtoto……..ila nawapa pole wafiwa….huwenda angekuja kuwa Makonda mpya au Lugola mpya….

  3. Nimemsikiliza kiranja wa shule ile na kilichoniuma sana ni kuwa mtoto huyu kuwa na nidhamu ndio kilichopelekea kifo chake kwani ilikuwa ni kawaida kuwapokea waalimu wake pindi alipoona wana mzigo. Na kiranja ameelezea wazi kuwa kipigo hakikuwa cha kawaida marehemu aliteswa sana kabla ya kifo chake. Kwangu mm binafsi nikisikiliza maelezo ya kiranja wa shule haiwezi kuwa bahati mbaya. Wakati kila mzazi anaomba Mungu mtoto wake awe na nidhamu basi nidhamu ya mtoto huyu ilipelekea kifo chake. Very sad.

  4. Mjinga nini mtoto alipigwa na mpini mwalmu alifikia a2a ya kuchukua bikari akamchoa kucha mtoto akaendelea kulalamika kua ajaiba pochi kiasi kwamba adi wenzake walichukia ndo maana alipo kosa nguvu akanunuliwa juis alikataa akasema sijiskii kunywa chochote ila mwalm ameniua kana kwamba alikua haumwi tena vilemtoto niyatima hana wazazi nyie acheni usenge maisha ya mtoto yanapotea kwa nidhamu yake mwenyewe

  5. Msenge kumamake wewe ujazaa nn msenge kweli mi mwanangu an image anaingia skull naletewa mait eti bahat mbaya wakat mmzamilia kwann pochi jaikupotea bahat mbaya mkakausha pochi inamanufaa kuliko roho mwenye pochi hajakausha mwenye mtoto akaushe wewe

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents