DStv Inogilee!

Show ya Akothee nchini Kenya yazua gumzo mtandaoni, Serikali yalaani uchafu aliufanya jukwaani

Msanii wa kike wa muziki nchini Kenya, Akothee ameingia kwenye headlines nchini humo baada ya kutumbuiza kwa staili ya aina yake kwenye jukwaani la show ya Valentines Beach Party iliyofanyika Wikiendi iliyopita katika fukwe za Paparemo mjini Watamu nchini humo.

Akothee aliyepanuliwa miguu katikati

Akothee kama iliyowasanii wengine, alianza kuposti kwenye mitandao ya kijamii picha za show ambazo nyingi ziliashiria uharibifu wa maadili na kuchochea ngono kama wadau wa mitandaoni walivyomshambulia.

Akothee akifanya yake jukwaani

Wazazi wake nao walikuwepo kwenye show

Wadau wengi mitandaoni nchini Kenya, wamelaani kitendo cha Akothee kutumbuiza jukwaani hadi kupitiliza.

Hata hivyo, sio Wakenya wote wamemponda wapo wengine wamefurahishwa na kitendo hicho kwa kuita kuwa ni ubunifu kwani hata Marekani wanafanya hivyo.

Hata hivyo, tayari Serikali kupitia kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza La kuthibiti Filamu nchini Kenya (KFCB), Dkt. Ezekiel Mutua imelaani kitendo hicho.

Dkt. Mutua amesema kuwa Akothee ni msanii mkubwa lakini kwa kiki zake anazofanya hawezi kufika popote, na kama ikiendelea hivyo basi hata kiwanda cha burudani nchini humo kitakufa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW