Burudani

Siku kama ya leo miaka 23 iliyopita, Dunia ilimpoteza mtu muhimu kwenye historia ya muziki wa Hip Hop duniani

Leo September 13 ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyewahi kuwa mwanamuziki nguli wa Hip Hop nchini Marekani, Tupac Amaru Shakur  ‘2 Pac’ ambaye alifariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

2 Pac

Mwanamuziki huyo alipigwa risasi mnamo tarehe 7 Septemba, 1996, Huko Nevada jiji la Las Vegas nchini Marekani na baadae siku 6 akafariki dunia akiwa anatibiwa majeraha  hospitalini.

Jina lake la kuzaliwa ni Tupac Amaru Shakur alizaliwa Juni 16, 1971, Na enzi za uhai wake aliwahi kuingia kwenye kitabu cha maarufu cha rekodi duniani cha “Guinness World Records” kutokana na mauzo ya album yake kutajwa kufikia milioni 74 Dunia nzima na milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee kama msanii wa muziki wa Hip Hop.

Majina mengine ya 2 Pac ni Makaveli na mashabiki wake wengi Jijini New York walimpa jina la ‘MC New York’ .

2 Pac alijizolea umaarufu mkubwa duniani kote kupitia kazi zake za muziki baada ya vibao vyake kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani na nje ya Marekani.

Baadhi ya nyimbo za 2 Pac zilizobamba wakati wa uhai wake ni Dear Mama, California Love, Life Goes On, Hit Em Up pamoja na Hail Maily ambazo zilikuwa moto wa kuotea mbali wakati huo.

2 Pac aliacha Studio Album 10 na alizowahi kutoa kabla ya umauti ni All Eyez On Me, The Don Killuminati: The 7 day Theory na Me Against The World.

Kifo cha 2 Pac kinahusishwa na ugomvi uliokuwepo kati yake na rapa mwenzake The Notorious B.I.G ambaye pia ni marehemu kwasasa.

2 Pac na B.I.G ni miongoni mwa wana Hip Hop walioleta mapinduzi makubwa enzi za uhai wao kwenye tasnia ya muziki nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents