Habari

Spika wa Bunge nchini New Zealand aushangaza ulimwengu, Afanya tukio lililosababisha Mbunge nchini Kenya afukuzwe bungeni

Spika wa Bunge nchini New Zealand, Trevor Mallard jana Agosti 20, 2019 ameishangaza dunia baada ya kumchukua mtoto wa Mbunge mwenzake wa upinzani bungeni, Tāmati Coffey na kuanza kumnywesha maziwa.

Spika Mallard wakati akiendelea kuruhusu maswali na majibu kutoka kwa mawaziri wawili wa Nishati na Biashara, Alisikika akimsifia mtoto huyo kuwa ni mzuri na hakuna tatizo lolote na kuwataka wabunge waendelee na mijadala bungeni.

Baba wa mtoto huyo, Tamati Coffey alisikika akimshukuru Spika wake bungeni baada ya kuambiwa kuwa amezaa mtoto mzuri na hakuna tatizo yeye kukaa naye mbele ya Bunge kwani kila mtoto ni zawadi kwa taifa hilo kutoka kwa Mungu.

Spika Mallard alikaa na mtoto huyo karibia muda wote wa kikao huku majadiliano makali yakiendelea bungeni.

Mtoto huyo aitwaye Tūtānekai Smith-Coffey amezaliwa mwezi uliopita kwa njia ya mama wa kukodi (surrogate mother), Licha ya kuwa yupo kwenye mahusiano na mchumba wake aitwaye Tim Smith.

Tāmati Coffey alifanikiwa kuingia bungeni mwaka 2017 kwa tiketi ya chama cha Labour, Baada ya kushinda ubunge katika jimbo la Waiariki  nchini humo.

Kazi nyingine iliyompa umaarufu zaidi nchini New Zealand ni Utangazaji ambapo amefanya kazi na kituo kikubwa cha runinga cha taifa hilo cha TVNZ na kutangaza mashindano makubwa ya New Zealand’s Got Talent.

Mwezi uliopita tukio kama hilo la kuingia na mtoto bungeni, Lililotokea nchini Kenya ambapo Spika wa Bunge aliamuru Mbunge mwenzake aliyeingia na mtoto bungeni atolewe upesi huku akidai kuwa bungeni sio sehemu ya malezi.

Katika tukio hilo, Ndg. Christopher Omulele, ambaye alikuwa anahudumu kama Spika alimuamuru Mbunge Zuleikha Hassan ambaye alikuwa ameingia na mwanae mwenye umri wa miezi mitano kuondoka bungeni, akisema kuwa bunge sio mahali sahihi pa kumlelea mtoto wake.

“Nimefukuzwa bungeni kwasababu nilimpeleka mtoto bungeni, Niliamua niende kazini na mtoto wangu, mtoto asingebaki peke yake, au nikae nae nyumbani nisiende kazini’,’ alisikika Bi. Zuleikha katika mazungumzo na kituo cha BBC baada ya kufukuzwa na mwanawe bungeni.

https://www.instagram.com/p/B1bsAiLBnKi/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents