Burudani

Star Wars: The Force Awakens aliyoigiza Lupita Nyong’o yaingiza $1bn siku 12 baada ya kuingia kwenye majumba ya sinema

Star Wars: The Force Awakens imekuwa filamu iliyoingiza dola bilioni 1 haraka zaidi kwenye majumba ya sinema duniani.

Star Wars The Force Awakens

Filamu hiyo ya JJ Abrams imefikia mafanikio hayo siku 12 tu baada ya kutoka na kuvunja rekodi iliyopita ya siku 13 iliyowekwa na filamu Jurassic World June, mwaka huu.

Hata hivyo Jurassic World ilipata mafanikio hayo kwa kuoneshwa China zaidi ambako The Force Awakens bado haijaoneshwa huko.

Star Wars pia iliingia fedha nyingi siku ya Christmas kwa Marekani kwa kuvuta $49.3m. Kwa upande wa Marekani pekee filamu hiyo imeingiza $544.6m.

Filamu hiyo iliyotayarishwa kwa bajeti ya dola milioni 200 imewakutanisha waigizaji mbalimbali wakiwemo Lupita Nyong’o, Harrison Ford, Mark Hamill, Carrie Fisher, Adam Driver, Daisy Ridley, John Boyega, Oscar Isaac, Andy Serkis, Domhnall Gleeson, Anthony Daniels, Peter Mayhew na Max von Sydow.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents