Tupo Nawe

TAFITI: Wanawake waliokwenye mapenzi na wanaume wadogo kiumri kuliko wao, Huridhika zaidi kwenye mahusiano

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mwanasaikolojia  Dkt. Justin Lehmiller umeonesha kuwa wanawake ambao wapo kwenye mapenzi na wanaume wenye umri mdogo kuliko wao, Wanaridhika zaidi kwenye mapenzi kuliko wale wanawake waliopo kwenye mapenzi na wanaume wenye umri mkubwa kuliko wao.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron (41) na mkewe Brigitte Macron 66

Dkt. Lehmiller amesema amefanya utafiti kwa wanawake 200, Ambao wote wapo kwenye mahusiano na kuwauliza wanavyoridhika kwenye mapenzi wakiwa na wenza wao.

Na matokeo yalionesha kuwa asilimia 70 sawa na wanawake 140 waliokuwa wamewazidi umri wanaume wao,  Walisema wanaridhishwa na wanafurahia mahusiano yao.

Asilimia 18 ya wanawake ambao walikuwa karibia sawa kiumri na wenza wao, Walisema mahusiano yao yapo kawaida na kuna muda yanabadilika.

Na, Asilimia 12 ya wanawake walio kwenye mapenzi na wanaume wenye umri mkubwa kuliko wao, Wamesema hawaridhiki kwenye mahusiano na wanakosa uhuru wakiwa faragha.

Akieleza sababu ya kwanini wanawake wenye umri mkubwa huridhika zaidi wakiwa kwenye mapenzi na wanaume wadogo kiumri, Dkt.  Lehmiller amesema “Siwezi kuzungumzia ni kwanini ila kutokana na utafiti wangu, Inaonesha wanawake wengi wanapenda usawa na kujiona wana nguvu kwenye mahusiano kuliko kuongozwa,“.

Hivyo  naamini, Mwanamke akiwa mkubwa kwenye mahusiano kuna hali hujisikia kutawala. Hiyo ndio sababu wanawake wengi wakubwa wanakuwa na furaha kwenye mahusiano na wanaume waliowazidi umri. Ingawaje itategemeana na huruka za mwanaume,“.

Dkt. Lehmiller ameendelea kueleza kwa kusema kuwa “Hii inakuwa ni ngumu kidogo kwa sababu, Wanaume wengi kwenye mahusiano wanataka kutawala na ndio maana wanachagua wanawake waliowazidi umri ambao mara nyingi wanakosa sauti, Hii inapelekea unyonge huo mpaka kwenye mapenzi wanakosa uhuru wa faragha.“.

Nchi za Ulaya ikiwemo Italia, Ufaransa, Sweden na Ireland ndio bara linaloongoza wanawake wakubwa kuolewa na wanaume wenye umri mdogo.

Bara la Afrika karibia nchi zote, Ndio linaongoza kwa wanawake kuolewa na wanaume waliowazidi umri. Sababu imetajwa kuwa ni tamaduni na umasikini.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW