Habari

Tahadhari ya mvua kubwa na mafuriko yatolewa (+video)

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa baadhi ya mikoa nchini kuwa kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika siku tano zijazo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na TMA jana Desemba 16, 2018, imeeleza kuwa wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kusini na karibu na Bahari ya Hindi kuchukua tahadhari hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kuanzia leo Jumatatu Desemba 17, 2018 hadi Desemba 20, 2018 baadhi ya mikoa itaathiriwa na mvua kali ambayo inaweza kupelekea mafuriko.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents