Habari

TAKUKURU yasema “Uchunguzi kuhusu Kangi Lugola, Andengenye na wengine wakamilika kwa asilimia 99 Uamuzi huu wachukuliwa” – Video

TAKUKURU yasema "Uchunguzi kuhusu Kangi Lugola, Andengenye na wengine wakamilika kwa asilimia 99 Uamuzi huu wachukuliwa" - Video

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU imesema uchunguzi wa sakata la manunuzi ya vifaa vya zimamoto na uokoaji yasiyozingatia sheria na taratibu za nchi ambao ulisimamiwa na aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani KANGI LUGOLA na aliyekuwa kamishna Jenerali wa jeshi la zimamoto THOBIASY ANDENGENYI umekamilika kwa asilimia 99.9

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, ameviambia vyombo vya habari kuwa uchunguzi umebaini makosa mengi katika mkataba wa manunuzi hayo ambayo kwa pamoja yanatengeneza kosa la uhujumu uchumi.

Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo TAKUKURU wanapeleka taarifa ya uchunguzi huo kwa mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali tayari kwa hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote 17 wa sakata hilo.

 

Kama hujafanikiwa kuitazama video ya Mbatia akiongea kuhusu kushirikiana na vyama vingine, Unaweza kutazama hapa chini.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents