Burudani

Tatizo la Umeme nchini Slovakia lasababisha show ya Nicki Minaj kuahirishwa

Ikiwa ni tour yake katika bara la Ulaya mwanadada Onika Tanya Maraj alimaarufu Nicki Minaj ambaye ni miongoni mwa marapper wa kike wanaofanya vizuri duniani akitokea nchini Marekani.

Kwa mujibu wa TMZ. Katika show yake ambayo angetakiwa kifanya jana nchini Slovakia Nicki Minaj hakuweza kufanya baada ya uwanja aliopangwa kufanyika kukumbwa na masuala makubwa yaliyo nje ya uwezo wake ikidaiwa tatizo kubwa lilikuwa ni umeme.

Lakini imeelezwa kuwa Nicki bado alihakikisha kutokuwaacha mashabiki waliofika hapo bila hata kuisikia sauti yake na badala yake mamia ya mashabiki wake aliamua kuwasalia kwa kupita pembeni.

Akieleza mmoja wa wahusika wa uwanja huo alisema ” Tunaambiwa transfoma imezima” … licha ya kuelezwa kuwa uwanja huo ulijaa sana. Masuala ya Umeme hayakuzuia Nicki kuwasalimia wale waliokuja kumwona. Minaj mwenyewe aliwaambia wasisikilizaji kile kilichokuwa kibaya … na alitumia masaa kadhaa kutembea karibu na uwanja na kusema hello.

Ikumbukwe kuwa Nicki bado ana maonyesho mengine 20 kwenye ziara ya Ulaya … na anapanga tarehe mpya kwa mashabiki wake nchini Slovakia.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents