Toronto Raptors wamaliza gundu la Drake, Mwenyewe atangaza habari njema, Stephen Curry amvulia kofia

Gundu lililokuwa linamuandama msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Drake huenda likawa limefikia ukomo kwani timu yake ya Toronto Raptors jana usiku imetwaa ubingwa wa NBA 2019.

Drake na Curry

Drake ambaye ni shabiki wa Toronto Raptors jana baada ya ushindi huo alionekana mtu aliyejawa na furaha, na kuahidi kuachia ngoma mbili ndani ya mwezi huu kama zawadi kwa mashabiki wa Raptors.

Tangu mwaka huu uanze, Drake amekuwa akitajwa kuwa msanii mwenye gundu, hii ni baada ya kila mwanamichezo aliyekuwa akipiga naye picha basi timu yake au klabu yake imekuwa ikipata matokeo mabovu.Image result for anthony joshua drake

Picha ya mwisho aliyopiga na Bondia Antony Joshua wiki iliyopita, ilisababisha pia bondia huyo kupigwa KO kwenye pambano lake na Andy Ruiz Jr .

Kutokana na hali hiyo, Klabu ya AS Roma ya Italia ilipiga marufuku wachezaji wao kupiga picha na mkali huyo wa hit song ya God’s Plan.

Kwa upande mwingine, Mchezaji wa Golden State Warriors, Stephen Curry amemtumia salamu za pongezi Drake mapema baada ya timu yake kunyukwa na Toronto na kuvuliwa ubingwa wa NBA 2019.

Kabla ya michezo hiyo ya fainali kuanza, Drake pia alipiga picha na Curry na kilichotokea Warriors wakapigwa na Toronto kwenye mchezo wa kwanza wa fainali hizo.

Ushindi wa Toronto Raptors wa jana usiku, umekuja baada ya kushinda michezo minne kati ya mechi 6 zilizopigwa huku Warriors wakishinda mechi mbili pekee.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW