Burudani

Tuhuma za ubakaji zaendelea kumkosesha raha mchungaji Fatoyinbo Nigeria, Umoja wa Makanisa waanza kumchunguza

Tuhuma za ubakaji zaendelea kumkosesha raha mchungaji Fatoyinbo Nigeria, Umoja wa Makanisa waanza kumchunguza

Mchungaji Biodun Fatoyinbo ameshindwa kufika katika mahojiano ya kutafuta ukweli kuhusu shutuma za ubakaji baada ya kuitwa katika kamati ya maadili na uchunguzi ya kanisa la pentecostal nchini Nigeria.
Msemaji wa taasisi hiyo anasema jitihada za kumpata mchungaji huyo zimegonga mwamba lakini walimpata mlalamikaji aliyewasili kuhojiwa akiwa na mumewe, hivyo mpaka sasa wana taarifa za upande mmoja pekee.


Mchungaji Fatoyinbo anashutumiwa na mpiga picha maarufu na mke wa mwanamuziki Timi Dakolo anayeitwa Busola kuwa alimbaka mara mbili kipindi ambacho binti huyo alikuwa na umri chini ya miaka 18.
Picha ya video ya mwanadada Busola Dakolo ilisambaa mtandaoni mwezi june akimshutumu mchungaji huyo kwa ubakaji.

Mchungaji huyo alipinga shutuma hizo, na polisi walisema hawakupata malalamiko yoyote kutoka kwa Bi.Dokolo.
Hata hivyo punde baada ya shutuma hizo kusambaa alilazimika kuachia wadhifa wake kutokana na kashfa hiyo.Kwa sasa umoja wa makanisa Nigeria 🇳🇬 umeanza kufanya uchunguzi wa shutuma hizo.

Yeye alikanusha kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii:-

https://www.instagram.com/p/BzQqv-CBmeV/

https://www.instagram.com/p/BzXkF8hBnSv/

Chanzo BBC.

https://www.instagram.com/p/B1fyi1wA3br/

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents