Fahamu

Ufahamu mji huu mkuu, ulioko barani Afrika usiokuwa na foleni

Mambo mengi tu ikiwemo mzozo na kutengwa kidiplomasia yamechangia pasi jitihada za makusudi mji mkuu wa Eritrea kuwa pepo ndogo ya uendeshaji baiskeli.

Kwa mujibu wa BBC. Asmara una wakaazi 500,000 wanaoishi katika mji huo, ambao ukiangazia na mishahara duni, kodi za kiwango cha juu za uingizaji biadhaa na uhaba wa mafuta una maanisha mji huo una magari machache. Na yale utakayoyaona huwa ni makuu kuu ya miaka ya nyuma.

Cyclists in Asmara, Eritrea
A donkey cart on a road in Asmara, Eritrea

Barabara ni tupu hazina magari mengi. Wakaazi wanalalamika kuondoka kwa idadi kubwa ya vijana ambao wameondoka katikamiaka 20 iliyopita kutokana na ugumu wa maisha unaotokana na mizozo na kulazimishwa kulihudumia taifa chini ya serikali ambayo sio kila mtu anakubaliana nayo.

Liberty Avenue in Asmara, Eritrea pictured in August 2018

Kutokana na hali hiyo, Asmara nimji wenye taswira tofauti na mataifa mengi barani Afrika yaliona msongamano wa magari na foleni zisizokwisha. Hii ikichanganywa na hali ya hewa nzuri, ni mzingira mazuri kwa raia kuendesha basikeli katika mji huo. “Uendeshaji baiskeli ni sehemu ya utamaduni wetu,” anasema mwanamume mwenye umri wamiaka 25.

A man on a bicycle riding past a street market in Asmara, Eritrea

Muundo wa ujenzi wa mji wa Asmara unwavutia wengi na hivi karibuni ulitangazwa kuwa kivutio duniani kwa sanaa iliyotumika katika usanifu wa majengo ya mji huo, utajiri ulioachwa katika wakati wa utawala wa kikoloni wa Italia kuanzia 1897 hadi 1943.

A street scene in Asmara, Eritrea

Madukaya kutengeneza baiskeli yametapakaa kila mahali Asmara. Eritrea ina historia ndefu ya kujitegemea ilioanza wakati wa vita vyake vya kupigania uhuru vya miaka 30 kutoka kwa Ethiopia, baada ya hapo kutengwa kimataifa kumefanya kuwa vigumu na ghali kuingiza vipuri na baiskeli mpya.

A bicycle repair stall in Asmara, Eritrea

Vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume nchini humo huendesha “bicicletta”, neno linalomaanisha baiskeli katika lugha ya Tigrinya, iliyotokana na lugha ya kiitaliano.

A man on a bicycle riding past a bike repair shop in Asmara, Eritrea
People with bicycles walking past street stalls in Asmara, Eritrea

Uendeshaji baiskeli pia una umaarufu miongoni mwa raia kutokan na kwamba nijambo lililoidhinishwa na Italia na mashindano ya uendeshaji baiskeli ni fahari kubwa miongoni mwa raia.

Timu ya taifa inayomjumuisha Mosana Debesay kwenye picha hii katika mashindano huko Austria Septemba mwaka jana, ina ufanisi mkubwa katika mashindano ya kimataifa.

Mosana Debesay of Eritrea at the 91st UCI Road World Championships 2018 on 25 September 2018 in Innsbruck, Austria

Maridhiano ya hivi karibuni baina ya nchi hiyo na Ethiopia yamewaacha raia wengi Eritrea wakitumaini kwamba uchumi utaimariki kwa kasi, na kurahisisha hali ya maisha Asmara.

x

Imeandikwa na mtaalamu wa masuala ya utu Milena Belloni na mwandishi James Jeffrey

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents