Tupo Nawe

Ugonjwa wa Malaria wabaki historia nchini Algeria na Argentina, Dkt. Kikwete atoa neno

Nchi za Algeria na Argentina zimethibitishwa rasmi na Shirika la afya duniani (WHO) kuwa zimetokomeza ugonjwa wa Malaria.

Kwenye taarifa hiyo iliyotolewa na WHO, imeonesha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita hakuna hata kisa kimoja kilichoripotiwa cha mgonjwa wa malaria katika nchi hizo.

Ugonjwa wa Malaria unaambukizwa kwa kuumwa na Mbu Jike na ni moja ya magonjwa yanayoongoza kwa vifo duniani.

Takwimu za mwaka 2017 pekee zilionesha visa Milioni 219 kuripotiwa na vifo zaidi ya Laki 4 vya Malaria, Huku 60% ya vifo hivyo vikiwa vya watoto wa umri wa chini ya miaka 5.

Kwa upande wa bara la Afrika, Algeria inakuwa nchi ya pili kutambuliwa  WHO kwa kutokomeza Malaria baada ya Mauritius ambayo ilithibitishwa rasmi mwaka 1973.

Kufuatia taarifa hiyo, Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Kikwete ametoa pongezi kwa mataifa hayo, kwa kufanikiwa kutokomeza Malaria.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW