Habari

Unahitaji shilingi ngapi ili uwe na furaha?

Je ni fadha kiasi gani inaweza kununua furaha yako? Kitu kikubwa ambacho kitapima furaha yako ni kuridhika na kufanikiwa kwa kile unachokifanya kazini kwako au kwenye biashara yako na maisha uliyonayo katika jamii inayokuzunguka. Fedha ni uwezo wa kununua vitu na mali, bali haiwezi kununua furaha ya mtu.

251505_474884312545591_766837583_n

Unapoweza kupata fedha ya kujikimu, mambo kama chakula, Mavazi, malazi, maji na umeme vingi vinavyokuja zaidi ya hapo ni ziada. Na vijana na watu wengi tumekuwa tukichukulia fedha kwa mtazamo tofauti na kujikuta tunafanya mambo ambayo ni magumu tukifikiria kwamba tunatafuta furaha. Tumeendelea kufanya kazi muda mrefu huku tukishindwa kujenga familia kimaadili, mahusiano na upendo kwa kisingizio cha kutafuta pesa na furaha zaidi. Kila kitu kinapoondoka kama ni mali na utajiri kinachobakia ni watu, hivyo jenga uhusiano mzuri na watu wanaokuzunguka na furaha unayoitafuta kwenye fedha haitakusumbua tena.

Unapochagua kazi kulingana na kiwango cha mshahara ukitegemea kuwa na furaha zaidi, unajidanganya kwa kuwa hautaridhika na fedha hiyo. Unahitaji kuridhika kwa kile unachokifanya na utaweza kupata furaha unayoitafuta.

Hakikisha una mahali pa kulala, umekula, umevaa, una maji na umeme  na utakuwa na furaha, tatizo ni kufuata mkumbo wa watu wengine wanaishije. Tunaporudi kwenye swali la msingi, unahitaji shilingi ngapi ili uwe na furaha? Inategemea na jamii uliokulia na namna walivyopotosha neno furaha, hivyo kuleta matatizo katika kufikiri kwako na jamii inayokuzunguka. Furaha yako haitapatikana  kwa kulazimisha kila mtu akuogope kwa fedha na mali, au dini, au elimu yako. Jitambue na uheshimu kwamba furaha inapatikana ndani yako mwenyewe endapo tu uwezo wako wa kufikiri utafikiri vizuri.

Maisha zaidi ya fedha, ni mtu kujitambua kwa kuwa thamani ya utu wako ni zaidi ya fedha unayofikiri itakupa furaha.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents