Habari

Usafiri wa Ndege waendelea kutia wasiwasi, Rubani aokoa maisha ya abiria 89 baada ya ndege kutua bila gurudumu la mbele baada ya hitilafu la kiufundi

Usafiri wa Ndege waendelea kutia wasiwasi, Rubani aokoa maisha ya abiria 89 baada ya ndege kutua bila gurudumu la mbele baada ya hitilafu la kiufundi

Rubani mmoja raia wa Myanmar alilazimika kutua bila gurudumu la mbele baada ya ndege kupata hitilafu ya kiufundi wakati wa kutua.

Ndege y atua ghaflaHaki miliki ya pichaNAY MIN
Image captionNdege y atua ghafla

Kwa mujibu wa BBC, Ndege hiyo ya shirika la ndege la Myanmar iliteleza kwa muda katika barabara ya ndege kabla ya kusimama katika uwanja wa ndege wa Mandalay.

Rubani wa ndege hiyo aina ya Embraer 190 alisifiwa kwa kutua salama na abiria wote 89 bila hata mmoja wao kujeruhiwa.

Kapteni Myat Moe Aung alizunguka uwanja wa ndege mara mbili ili kuwaapa muda waelekezaji wa ndege kutabaini ikiwa kifaa hicho kingeliweza kufanya kazi, ilisema shirika hilo la ndege.

Ndege hiyo iliyokuwa safarini kutoka Yangon na ilikuwa imepangiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mandalay lakini rubani alipojaribu kutua alishindwa kufanya hivyo kutokana na sababu za kiufundi.

Ndege y atua ghaflaHaki miliki ya pichaNAY MIN
Image captionNdege y atua ghafla

Rubani alifuata taratibu zote za kiusalamaikiwa ni pamoja na kumwaga mafuta zaidi ili kupunguza uzani wa ndege, ilisema shirika hilo la ndege.

Kanda ya video inayoonesha ndege hiyo ilivyotua kwa miguu yake ya nyuma kabla ya kugonga chini kwa pua.

Ndege hiyo iliteleza katika barabra ya ndege kwa sekunde 25 kabla ya kusimama.

“Rubani amefanya kazi kubwa sana,” Win Khant, Waziri wa uchukuzi wa Myanmar, aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kisa hicho ni ajali ya pili kutokea nchini Myanmar wiki hii. Siku ya Jumatano, ndege ya shirika la ndege la Bangladesh iliteleza na kutoka katika barabara ya ndege ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Yangon na kuwajeruhiwatu 17.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents