Tupo Nawe

Vanessa Mdee kuiwakilisha Tanzania kwenye meza ya majaji wanne wa shindano la East Africa’s Got Talent

Msanii muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ataiwakilisha Tanzania kwenye meza ya majaji wanne waliotangazwa na waandaaji wa shindano la East Africa’s Got Talent 2019.

Majaji wengine watatu waliotangazwa jana watakaosimamia shindano hilo kwa msimu wa kwanza ni mtangazaji wa runinga kutoka Kenya,  Jeff Koinange, Gaetano Kagwe (Uganda) na Contact Makeda (Rwanda).

Shindano hilo litaanza kuonyeshwa mwezi Agosti 4, mwaka huu kwenye vituo mbalimbali vya runinga hapa Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW