Habari

Video: Chadema yasema ina wajibu wa kuikosoa serikali

Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), kupitia Naibu Katibu Mkuu wake, Zanzibar, Salum Mwalimu amesema wao kama cha kikubwa cha upinzani wana wajibu mkubwa na mpana wa kuikosoa serikali iliyo madarakani.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu amesema wao zimekuwepo juhudi kubwa sana za kutaka kuwaziba midomo hawatozima midomo.

“Sisi kama kikubwa cha upinzani tuna wajibu mkubwa sana na mpana sana wa kuwazungumzia Watanzania bila kujali ni wa wapi, lakini sisi kama chama kikuu pia tuna wajibu wa kisheria kikanuni na taratibu zinazoongoza vyama vya siasa kuikosoa serikali iliyo madarakani au chama chochote kingine cha siasa,” alisema Mwalimu.

“Kwasababu shabaha yetu sisi kama chama kikubwa cha siasa ni kushika dola na huwezi kumpigia makofi hata yasiyo ya ulazima wala yasio na mantiki yoyote yule ambaye yupo madarakani, zimekuwepo juhudi kubwa sana za kutaka kutuziba midomo na sisi tunaendelea kuwaambia hatutozimika midomo hatutojali risasi wala mitutu ya bunduki, hatutojali jela kwasababu wote tumeubwa siku moja na kuzaliwa siku moja na tutakufa siku moja hakuna anejua atakufa kwa utaratibu gani.” 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents