HabariUncategorized

Video: RC Ayoub na mikakati ya usafiri kwa walimu, wanafunzi na wenye ulemavu

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib, Ayoub Mohamed Mahamoud amebainisha moja ya changamioto kubwa katika kisiwani Zanzibar ni suala la usafiri kwa wanafunzi, walimu na watu wenye ulemavu.

Akiongea na waandishi wa Habari, RC Ayoub ameeleza kuwa tayari serikali imeshapata muafaka wa suala hilo ambalo ni kuhakikisha kila mmoja wao naweza kuondokana na adha hiyo.

“Kwa upande wetu wa Zanzibar changamoto ni wanafunzi, sasa changamoto ya wanafunzi tayari imeshapatiwa ufumbuzi,Serikali imeshaweka ile ada iwe na utaratibu maalum lakini tunachokifanya kwanza ni kuangalia ni mfumo mzima wa usafiri kwa Mkoa wetu,” amesema RC.

Akaongeza “Kabla ya kuelekea kwenye taratibu ambazo wenzetu Dar Es Salaamu wameshaweza na DART,kwa mfumo wa usafiri na wameweza kutoa vitambulisho, lakini sisi muoelekeo wetu ni wamaeno matatu, kwenye usafiri mbali ya walimu, kuna wanafunzi na walemavu ili haya yake vizuri lazima tuweke mfumo wenyewe wa usafiri ndani ya Mkoa kwa sababu nao haujakaa vizuri.”

Akasisitiza “Nadhani mnaona wote pale Kisiwandui, kila siku kuna msongamano mkubwa sana ndiyo maana tunajaribu kufanya marekebisho eneo la Kijangwani, ili sasa zile daladala ziende Kijangwani zikienda kule ule mfumo utakaa vizuri na sasa trutakuja kwenye mfumo wenyewe ikiwemo suala hilo la walimu, wanafunzi na walemavu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents