Burudani

VIDEO: Wema Sepetu aburuzwa Mahakamani, afanikiwa kupata dhamana kwa masharti magumu (+video)

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo Novemba 01, 2018 ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam baada ya kuburuzwa mahakamani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya Kusambaza picha za faragha mtandaoni.

Wema Sepetu alipata dhamana mahakamani hapo baada ya kukidhi vigezo, ambapo moja ya sharti lilikuwa ni kupata mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Milioni 10.

Sharti lingine alilopewa kwenye dhamana hiyo, ni kutoposti picha au video zenye maudhui ya ngono kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu akiwa mahakamani hapo amekana shtaka hiloo, na kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa tena Novemba 20 mwaka huu.

Kwa upande mwingine, Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka watanazania kuacha kuweka picha za ngono mitandaoni kwani watakumbwa na mkono wa kisheria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents