Burudani ya Michezo Live

Vifahamu Vifo 11 vya watu weusi Marekani, Vilivyowahi kusababisha maandamano ya raia dhidi ya polisi

Kifo cha Mmarekani mweusi ambayealikamatwa na polisi akiwa hana silaha lakini polisi alionekana kutumia nguvu kwa kumkaba shingo na hivyo suala la ubaguzi dhidi ya jamii ndogo ya watu weusi ikaibuka.

George Floyd, aliyekuwa na umri wa miaka 46-alikuwa anafanya kazi ya ulinzi katika mgahawa mmoja wa Minneapolis, alifuatwa na polisi ambao walikuwa wanamtafuta mshukiwa wa mashtaka ya kughushi siku ya Ijumaa Mei, 25.

Video ya dakika 10-ambayo ilipigwa na shuhuda inaonyesha Floyd akimlalamikia afisa wa polisi akisema ” siwezi kuhema”.

Video ya tukio hilo lilisambaa kwa watu siku hiyohiyo ikionyesha mwanamke wa kizungu nchini Marekani akiwa anajibizana na mwanaume mweusi kuhusu mbwa wake ambaye alikuwa amefunguliwa.

Zaidi ya watu 1000 wameuwawa na polisi mwaka 2019

Kifo cha Floyd kimeweza kuibua hofu ya takwimu za mauaji ya polisi dhidi ya raia weusi nchini Marekani.

George Floyd pinned down

Kwa mujibu wa takwimu zilizowekwa na gazeti la Washington, watu 1014 walipigwa risasi na polisi katika taifa hilo kwa mwaka 2019, na utafiti unaonyesha kuwa wamarekani weusi ndio wahanga wakubwa.

Utafiti uliofanywa na asasi ya isiyokuwa ya kiserikali unadai kuwa katika vurugu ya polisi watu weusi wako katika hatari ya kuuwawa mara tatu zaidi ya watu weuse.

Uonevu wa Polisi umepelekea kuwepo kwa harakati za thamani ya utu wa mtu mweusi kuepo #BlackLivesMatter movement.

Watu maarufu kama muimbaji Beyonce na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Lebron James wameanzisha kahamasisha kampeni hizo kwa umma.

Hawa ni baadhi ya wahanga wengi wa vifo vilivyosababishwa na maandamano dhidi ya vurugu za polisi.

Trayvon Martin, 26 Februari 2012

Picture of Trayvon Martin

Trayvon Martin, a black 17-year-old high school student, was shot dead by George Zimmerman in Sanford, Florida.

Trayvon Martin, kijana mweusi mwenye umri wa miaka 17-alikuwa mwanafunzi wa sekondari. Alipigwa risasi na George Zimmerman huko Sanford, Florida.

Martin alikuwa anaenda kutembelea ndugu zake , lakini alipofika getini akakabiliwa na Zimmerman, raia wa Uhispania ambaye alikuwa alikuwa analinda maeneo ya jirani.

Mwaka 2013, mahakama ilimkuta Zimmerman kuwa hana hatia – sheria ya Marekani inamruhusu kumpiga risasi t Trayvon kwa lengo la kujihami, lakini familia ya kijana huyo na marafiki wanasisitiza kuwa ameuwawa.

Mauaji hayo ilionyesha wazi kuwa harakati za kijamii kuhusu thamani ya maisha ya watu weusi ni muhimu.

Eric Garner, 17 Julai 2014

Eric Garner

Garner alifariki kwa kukosa hewa baada ya kukamatwa kwa kushukiwa kuwa anauza sigara .

Video ilionyesha Garner akilia na kurudia kusema “siwezi kupumua” wakati afisa polisi wa kizungu , Daniel Pantaleo, alionekana akiwa amemkaba shingo Garner ambaye alikuwa anahangaika sakafunii.

Hukumu ilikanusha madai dhidi ya afisa huyo Pantaleo, kusababisha maandamano kadhaa katika nchini Marekani.

Pantaleo alifukuzwa kazi katika idara ya Polisi kwa kipindi cha miaka mitano baada ya tukio hilo kutokea.

Michael Brown, 9 Agosti 2014

Michael Brown

Harakati za maisha ya watu weusi ziliongezeka kuonekana kimataifa baada ya kijana mwenye mweusi mwenye miaka 18- Michael Brown kupigwa risasi na kuuliwa baada ya kuzozana na polisi wa kizungu Darren Wilson.

Tukio la Ferguson, Missouri, liliweza kuibua maandamano ya ghasia ambayo yalisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wengi kuumia na mamia kukamatwa.

Maandamano zaidi yalitokea mwezi Novemba mwaka huo huo baada ya mahakama kuamua kuwa Wilson ,ambaye alikuwa ameacha kazi ya polisi hana hatia.

Walter Scott, 4 Aprili 2015

Walter Scott

Walter Scott, alikuwa mwanaume mweusi mwenye miaka 50-, alipigwa risasi mwara tatu wakati akiwa anamkimbia afisa polisi Michael Slagger huko magharibi mwa Charleston, South Carolina.

Afisa polisi alisimamisha gari la Scott kwa sababu gari hilo lilikuwa lina taa za breki ya gari ambazo zina itilafu.

Wakati huo , Scott likuwa na hati ya kukamatwa kwa kosa la kuchelewa kutoa malipo ya huduma ya mtoto wake.

Slagger alikamatwa na kutakiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani mwaka 2017, huku familia yake ilipewa dola milioni 6.5 kutoka mamlaka ya magharibi mwa Charleston .

Freddie Gray, 12 April 2015

Freddie Gray

Kama wiki mbili hivi baada ya kupigwa risasi kwa Walter Scott, tukio lingine la kusikitisha lilitokea Baltimore, Maryland.

Kijana wa miaka 25- Fred Gray alikamatwa kwa kubeba silaha baada ya polisi kukuta kisu katika mfuko wake.

Video iliyopigwa na shuhuda inaonyesha Gray akipiga kelele akiwa amepakizwa kwenye gari la polisi. Saa chache baadae baadae alipelekwa hospitalini akiwa majeraha makubwa. Alifariki baada ya wiki na vurugu za maandamano zilitokea na polisi wapatao 20 walijeruhiwa.

Afisa watatu kati ya sita walihusika katika kukamatwa kwake ambapo hapo baadae walikutwa hawana hatia kwa kifo chake na wengine watatu hawakupelekwa mahakamani.

Placard with Sandra Bland's face

Sandra Bland, 13 Julai 2015

Bland alikuwa na miaka 28- alisimamishwa na askari wa jimbo la Texas Brian Encinia kwa makosa madogo ya kuvunja sheria za barabarani.

Wakati anamkaribia askari huyo aliwasha sigara na kukataa kuizima na kuitupa. Bland alikamatwa kwa makosa ya kumdharau afisa polisi baada ya maandamano dhidi ya operesheni hiyo kuanza.

Siku tatu baadae , alijiua akiwa gerezani. Wakati Bland hakuuliwa na polisi kwa vitendo lakini kifo chake kilisababisha maandamano nchini Marekani .

Kesi yake ilijulikana kama #SayHerName, harakati ambazo zilielezea unyanyasaji wa polisi dhidi ya binti mweusi .

Bland alikuja kuwa pia maudhui ya makala iliyorushwa na ‘ American cable network HBO’ mwaka 2018.

Philando Castile, 6 Julai 2016

Philando Castile's grave

Castile alipigwa risasi na polisi Jeronimo Yanez baada ya kusimamishwa na trafiki huko Minnesota.

Maombolezo yake yaliwekwa mubashara na mpenzi wake .

Ingawa Yanez alihukumiwa kwa udhalilishaji wa kiwango cha pili na makosa mawili ya kutokuwa makini na kwa silaha, baadae alihukumiwa kwa kifungo cha chini ya mwaka mmoja.

Botham Jean, 6 Septemba 2018

Botham Jean

Jean, 26, aliuwawa akiwa katika makazi yake na polisi wa kizungu ambaye hakuwa zamu Amber Guyger.

Afisa huyo alidai kuwa aliingia katika nyumba ya Jean kwa bahati mbaya kwa kudhani kuwa ni yake na alimpiga risasi Jean,ambaye hakuwa na silaha kwa kuamini kuwa mwizi.

Mwaka mmoja baadae, Guyger alihukumiwa miaka 10 gerezani.

Atatiana Jefferson, 13 Oktoba,2019

Atatiana JeffersonHaki miliki ya pichaFACEBOOK

Mwanafunzi wa udaktari, 28- Jefferson alipigwa risasi na kuuwawa akiwa chumbani kwake huko Forth Worth, Dallas, na afisa polisi officer Aaron Dean.

Dean alitumwa katika makazi yake baada ya majirani kutoa taarifa kuwa mlango wa mbele wa Jefferson’ ulikuwa wazi, na hivyo alimpiga risasi akiwa dirishani.

Afisa huyo alishtakiwa kwa mauaji lakini badokesi yake haijasikilizwa mahakamani.

Breonna Taylor, 13 Machi 2020

Breonna Taylor

Breonna Taylor, 26-alikuwa fundi mitambo ya dharura ya afya,alipigwa risasi mara nane wakati maofisa polisi walipoingia katika makazi yake huko Louisville, Kentucky, Machi 13.

Walikuwa wana kibali cha kuchunguza dawa lakini hakuna dawa ambazo zilipatikana katika vitu vyake.

Familia ya Taylor waliamini kuwa walikuwa hawamtafuti mpenzi wake lakini walikuwa na wanamtafuta mshukiwa ambaye tayari alikuwa amekamatwa na hakuwa akiishi katika gorofa hilo.

Polisi wa Louisville walidai kuwa waliamua kupiga risasi baada ya afsa mmoja kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katika tukio hilo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW