Habari

Wanahabari watakiwa kuzifanyia tafiti habari zao, kuzingatia maadili

MENEJA Miradi na Mikakati wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Sylvia Daulinge amewataka waandishi wa habari nchini kuhakikisha habari wanazozipeleka kwenye jamii ni za kweli, zilizofanyiwa tafiti za kina na zenye kuzingatia maadili.

Daulinge ameyabainisha hayo hivi karibuni na wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na chama hicho kupitia mradi wa ‘Media Science Café’ kuhusu namna bora ya kuripoti habari za afya kwa kuzingatia takwimu na maadili pamoja na jinsi ya kutumia majukwaa ya kidigitali kusambaza ajali wakati wa mgonjwa ya milipuko.

Alisema waandishi wa habari ni nguzo muhimu ya kuelimisha, kufundisha na kuhabarisha jamii taarifa mbalimbali ambazo ni za kweli na sahihi.

“Juzi juzi hapa tuliona athari za mvua na kulikuwa na taarifa nyingi ila waandishi wa habari katika kutoa habari hizo ni lazima tuzingatie ukweli, tafiti na maadili katika kupeleka taarifa kwa jamii,” alisema

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Dk. Rode Reuben

Aidha alisema ni muhimu waandishi kutumia majukwaa ya kidigitali katika kupata habari na kuhabarisha umma taarifa mbalimbali hasa za magonjwa ya milipuko.

Naye mtaalamu wa data kutoka Kampuni ya Habari na Teknolojia ya Nukta Africa, Daniel Samson alisema kama ilivyo kwa kuhakiki ukweli, uandishi wa habari kwa kutumia data ni moja ya jambo muhimu katika kuripoti habari hasa zinazohusu afya.

“Wote tunafahamu dunia inavyokua kwa kasi, suala la uandishi wa hadari za takwimu halikwepeki. Ukweli na usahihi unakua wa uhakika na kufanya mambo mengi yaeleweke zaidi kwa kutumia data,” alisema Samson

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Media Convergency (TMC0, Asha Abinallah alisema kujenga wasifu imara mtandaoni ndio humpa mwandishi wa habari nafasi ya ushindani na kujitofautisha katika zama hizi za maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha Abinallah aliwataka waandishi wa habari kuendelea kujifunza kwani wakifanya hivyo wanaongeza kitu kipya na wanaweza kuwa bora zaidi.

Naye Mhariri Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa ResearchCom, Shirika la mawasiliano la utafiti, Syriacus Buguzi alisistiza kuwa ni muhimu waandishi wanapopata habari kutoka sehemu fulani kabla hawajaziandika na kuziripoti kwa jamii ni vema kuzifanyia utafiti ili kuepusha sintofahamu.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents