Tupo Nawe

Wagombea vyama vya upinzani waliojitoa uchaguzi Serikali za Mitaa warudishwa ulingoni ‘Hakuna kukimbiana, Lazima kieleweke ‘

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwa wagombea wote wa upinzani ambao walioteuliwa na vyama vyao na kuwasilisha fomu za uchaguzi wataenda moja kwa moja kwenye kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa isipokuwa wale ambao wamekiuka kanuni za uchaguzi.

Image result for jafo
Selemani Jafo

Waziri Jafo ametoa jauli hiyo leo Jumapili Novemba 10, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusiana na mwenendo wa Uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wagombea waliochukua fomu na kuzirejesha wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi na nimefuta maamuzi yote yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi kote nchini ya kuwaengua wagombea wa vyama mbalimbali” Mhe. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Hata hivyo, Jafo amesema uamuzi huo hautawaruhusu wagombea ambao si raia wa Tanzania na wale ambao hawajajiandikisha katika kijiji, mtaa ama kitongoji husika.

Wengine ambao hawatahusika ni waliojiandikisha kupiga kura mara mbili, waliojidhamini wenyewe, hajadhaminiwa na chama chake cha siasa, wamerejesha fomu watu zaidi ya mmoja kutoka chama kimoja kwa nafasi inayofanana ya mwenyekiti wa kijiji, mtaa au kitongoji kwa kijiji, mtaa, au kitongoji husika.

Na lingine ni mgombea aliyejitoa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Tangazo la Serikali Namba 3.71 la Mwaka  2019 kanuni ya 19.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW