Habari

Wahandisi washauri watakiwa kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa barabara nchini

Naibu Katibu Mkuu anayesimamia miundombinu OR-TAMISEMI Mhandisi Rogatus Matavila amewataka Wahandisi Washauri wanaosimamia miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara nchini kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.

Mhandisi Matavila ameyasema hayo leo tarehe 10 Juni,2024 wakati akikagua ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi katika manispaa ya Tabora ambalo lipo chini ya mradi wa TACTIC inayosimamiwa na TARURA.

“Mhe. Rais anahangaika kutafuta fedha ili kuhakikisha wananchi wanapata barabara,wataalamu lazima mbadilike na kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa miradi hii. huyu angekuwa anasimamiwa kwa ukaribu angeshakuwa amemaliza hapa”.

Hata hivyo Mhandisi Matavila amewataka wataalam hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa ujenzi ili wakandarasi wakamilishe kazi kwa wakati.

Aidha, amemtaka Mhandisi Mshauri UNITEC Civil Consultants ltd kuhakikisha anasimamia kwa karibu ujenzi huo na ifikapo mwezi Agusti mwaka huu jengo hilo liwe limekamilika

Ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi linalogharimu takriban milioni 800 lilianza ujenzi wake Novemba 2023 na lilitarajiwa kukamilika 15 Juni,2023 na kuagiza ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Agosti 2024 na linajengwa na mkandarasi CICO Contractor.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents