Habari

Wamiliki mabucha watumia dawa ya kuhifadhia maiti kuhifadhi nyama isioze

 

Unaambiwa ukistaajabu ya Musa basi utajionea ya Filauni! kumekuwa na taarifa kuwa kuna baadhi ya maeneo nchini Uganda watu wanaomiliki mabucha wamekuwa na desturi ya kutumia dawa ya kuhifadhia maiti kwa kuhifadhia nyama iliyobaki ili isioze.

 

Sasa ukweli ni serikali nchini humo jana alhamisi januari 11, 2017 imefanya msako mkali kwenye Mabucha mjini Kampala ili kubaini  baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia dawa hatari zikiwemo za kuhifadhia maiti na zile za kuulia wadudu.

Imeelezwa kuwa Wafanyabiashara hao wanadaiwa kutumia kemikali hizo ili kuhifadhi nyama zisiharibike na waweze kuuziuza kwa muda mrefu.

Katika oparesheni hiyo mabucha tisa jijini Kampala yameshafungwa kwa kutumia madawa ya aina hiyo ambapo kama itabainika kwenye upelelezi watapelekwa Mahakamani.

Ni lazima watunze sehemu zao za kuuzia nyama (Mabucha) kuwa safi na kuacha kutumia madawa yasiyostahiki  la sivyo tutawapeleka mahakamani,“amesema Msemaji wa Mamlaka ya Uangalizi wa Jiji la Kampala (KCCA), Pater Kauju kwenye mahojiano yake na BBC.

Madhara ya kutumia nyama iliyohifadhiwa na madawa ya kuhifadhia mauti ni makubwa ikiwemo kuuwa viungo na seli mbalimbali mwilini.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents