Burudani ya Michezo Live

Wanaijeria 80 wakamatwa Marekani kwa udanganyifu wa mapenzi mtandaoni, Yadaiwa wameliingizia taifa hasara ya Tsh. Bilioni 328

Watu 80 wengi wao wakiwemo ni raia wa Nigeria wamekamatwa Los Angeles nchini Marekani kwa kujihusisha na biashara za udanganyifu wa kimapenzi mtandao.


Maafisa wa FBI ambao ndio waliowakamata waharifu hao, Wameonya kuwa kashfa na udanganyifu huo wa kimapenzi mtandaoni umeigharimu Marekani fedha nyingi kuliko kosa lolote la udanganyifu lililoripotiwa kwao mwaka jana.

FBI wamekadiria kuwa zaidi ya watu 21,000 walidanganywa na kutuma jumla ya Dola Milioni $143 ambayo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 329 kwa mwaka 2018.

Wezi hao wapo zaidi kwenye Apps za kimahaba ‘Dating Apps’  na kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook.

Watuhumiwa wote waliokamatwa watakabiliwa na mashtaka  ya kula njama za kulaghai na kutakatisha fedha na wizi wa utambulisho.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa FBI, Paul Delacourt amesema kuwa waliotapeliwa walitumika kama wasafirisha fedha ambapo waliruhusu akaunti zao kusafirisha fedha zilizoibwa.

Chanzo: https://www.aljazeera.com/news/2019/08/charges-80-people-nigerians-46m-internet-scam-190823071850782.html

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW