Habari

Watu 12 wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi uliofanyika katika jumba la serikali Virginia nchini Marekani

Watu 12 wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi uliofanyika katika jumba la serikali Virginia nchini Marekani

Watu 12 wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi uliofanyika katika jumba la serikali katika jimbo la Virginia nchini Marekani, polisi wamesema. Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshukiwa ambaye ni mfanyakazi wa muda mrefu katika kituo cha manispaa ya Virginia , alifyatua risasi kiholela .

Kwa mujibu wa BBC. Mshukiwa huyo ambaye hakutajwa aliuawa baada ya polisi kuwasili katika eneo hilo na kumkabili.

ruhiwa baada ya risasi kupiga nguo yake ya kuzuia risasi”, alisema afisa Cervera.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanaamini kwamba mshambuliaji huyo alikuwa peke yake. Lengo la mtu huyo bado halijatambuliwa.

Eneo la kandokando ya jumba hilo, lenye majumba mengi ya serikali lilifungwa na wafanyikazi wa serikali kuondolewa.

”Tuliwasikia watu wakipiga makelele, wakiwataka watu kutoka ndani ya majumba hayo ”, Megan Banton , msaidizi mmoja katika jumba hilo aliambia kituo kimoja cha runinga kwa jina WAVY.

Ramani inayoonyesha sehemu ya ufukwe wa eneo la Virginia Beach

“Haya ni maafa mabaya kwa wakaazi wa Virginia beach” , alisema gavana wa Virginia Ralph Northam katika mtandao wa Twitter.

”Moyo wangu unawalilia waathiriwa wa shambulio hilo na wale wote waliowapenda. Naelekea Virginia Beach kwa sasa na nitawasili katika kipindi cha saa moja baadaye”.

Meya wa Virginia Beach Bobby Dyer alielezea tukio hilo kuwa baya zaidi katika historia ya mji huo.

Maafisa wa Ujasusi wa FBI walikuwa katika eneo hilo kuwasaidia maafisa wa serikali za mtaa kuchunguza shambulio hilo kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Kulingana na mtandao wa Marekani wa Gun Violence Archive hili ni shambulio la 150 kufanyika nchini Marekani mwaka huu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents