Habari

Watu watano wafariki dunia baada ya lori na gari ndogo kugongana na kuwaka moto

Watu watano wafariki dunia baada ya lori na gari ndogo kugongana na kuwaka moto

Watu watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana na kupinduka, kisha moja kuteketea kwa moto wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Taarifa ya polisi inasema Lori linalomilikiwa na kampuni ya Dangote lenye namba za usajili T 191 DKT lililokuwa likitokea Mkuranga kuelekea Kibiti liligongana na Gari dogo lenye namba T 105 DGX T/Premio na kupinduka kisha kuwaka moto baada ya kupoteza muelekeo na kugonga nguzo ya umeme iliyopelekea gari hilo kuwaka moto na kusababisha vifo kwa watu watano, kati yao, wanne walikuwa katika lori la Dangote.

Kwa mujibu wa Azam Media: Miili ya marehemu imepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi, wakati dereva wa gari dogo anapatiwa matibabu hospitali ya Misheni ya Mchukwi.

https://www.instagram.com/p/B10uA1VgunN/

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents