AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Waziri Kigwangalla amvulia kofia Rais Magufuli ‘utake usitake, uthubutu wake ni wa dunia nyingine’

Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameguswa na uthubutu wa Rais Magufuli wa kununua ndege mpya kwa lengo la kukuza shirika la ATCL.

Image result for kigwangalla rais Magufuli
Waziri Kigwangalla

Waziri Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Facebook, amesema kuwa Tanzania ilihitaji Rais kama Dkt. Magufuli na amepatikana kwa muafaka.

“‪Uthubutu wa Rais Magufuli ni wa dunia nyingine. Utake usitake, umpende umchukie, kazi yake utaikubali tu! Tulihitaji Rais wa aina hii kwa wakati huu, Mungu ametupa! Alhamdulillah 🙏🏿.“ameandika Waziri Kigwangalla.

Waziri Kigwangalla kwenye posti hiyo, ameweka pia video ya ndege mpya aina ya Airbus A220-300, ambayo inatarajiwa kutua nchini siku yoyote kuanzia leo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW