Habari

Waziri Lugola asema Tundu Lissu ni mzururaji akamatwe, CHADEMA wamjibu

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ameshangaa Jeshi la Polisi kushindwa kumkamata mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kwa kudai kuwa Mbunge huyo amepona na amekuwa mzururaji nje ya nchi.

Image result for kangi lugola vs tundu lissu
Waziri Kangi lugola

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo jana Februari 13, 2019 jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake mkoani humo na kuelezea tukio la mwanasheria mkuu huyo wa Chadema kupigwa risasi jijini Dodoma mwaka 2017.

Kama amepata nafuu (Lissu) badala ya kuanza uzembe wa uzururaji alipaswa kuja (nchini). Nashangaa Polisi kila siku wanahangaika kukamata vijana kwa uzururaji na kumuacha huyu (Lissu),” alisema Lugola.

Kwa upande mwingine, Waziri Lugola amehoji kuhusu dereva wa Tundu Lissu kutopatwa na madhara ile hali gari lake lilipigwa risasi zaidi ya 30.

Kwa hali ya kawaida tu ni jambo la kushangaza, risasi zote hizo wanasema 38 hakuna hata iliyomgusa (dereva),” amesema Lugola.

Hata hivyo, leo Februari 14, 2019 CHADEMA wamejibu kauli hizo mbele ya waandishi wa habari kwa kusema Lissu anachokifanya kule nje ni jambo zuri na hachafui nchi.

Anayechafua nchini ni nani? mambo anayoyasema nje kule ni ukweli. Anayechafua nchi au serikali ni yule anayefanya haya mambo.“amesema Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa CHADEMA na kumjibu Lugola.

Serikali isije na propaganda, inatakiwa kuchunguza hili suala. Hili suala la (kushambuliwa kwa Tundu lissu) linatakiwa lichunguzwe, ikibidi serikali iombe hata msaada kutoka Jumuiya za kimataifa.. Kwa hiyo tunataka serikali itoke iseme imefanya uchunguzi hadi wapi? na sio propaganda,“.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents