Burudani

Milioni 50 tulizopewa zimetusaidia kufungwa bao moja, pengine tungefungwa hata 6 – Waziri Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka kwa mara ya kwanza kuelezea kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Taifa Stars dhidi ya Lesotho.

Image result for waziri mwakyembe Taifa Stars

Waziri Mwakyembe akiongea na Waandishi wa Habari mapema jana baada ya mchezo huo, amesema kuwa akifika Tanzania, atamwambia Rais Magufuli “tumefungwa bao moja na tunasubiri mechi ya Uganda ambayo lazima tushinde, huu ndiyo moyo wa kimchezo,  ukijikunyata utakuwa unadundwa ngumi kila wakati”.

Akielezea kuhusu zile Milioni 50 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya kuisaidia Taifa Stars,  Waziri Mwakyembe amesema “Milioni 50 tulizopewa zimetusaidia kufungwa bao moja tu, pengine tungefungwa hata sita. Tumefungwa sawa ndiyo mchezo tunaendelea kutafuta ushindi, tumejitahidi sana ila kwa sasa sio kichwa cha mwendawazimu tena,”.

Kwenye mchezo huo uliopigwa jana, Rais Magufuli alikuwa ni moja ya Watanzania waliokuwa wanafuatilia mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents