Burudani

Wema Sepetu ‘kuamsha dude’ Aprili 26 mkoani Arusha

Muigizaji wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu atakutana na mashabiki wake pamoja na wakazi wote wa Arusha kwa siku mbili mfululizo kuwauzia bidhaa zake mpya za Lipsticks ambazo mashabiki wake walizimiss kwa miaka miwili.

Wema Sepetu

Kupitia tangazo lake alilochapisha kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema amesema kuwa ataanza kuuza bidhaa hizo mkoani Arusha kwa siku mbili kuanza tarehe 26 hadi 27 Aprili 2018, ambapo yeye mwenyewe ndiye atakayekuwa anahudumia wateja watakaokuwa wanahitaji huduma, katika duka la Kubrasadiki.

Good News For you, Tunakuja week hii tar 26 na 27… Tutakuwepo kwenye Duka la Wakala wetu Mkubwa wa Arusha @kubrasadiki @kubrasadiki @kubrasadiki. Na nitakuuzia Lipstick mwenyewe… Cant wait kumeet warembo wangu…. Alhamis na Ijumaa hii Ladies & Gents.“ameeleza Wema Sepetu.

Wema Sepetu ametangaza kurudisha bidhaa zake hizo za Lipstick sokoni baada ya kusimama kwa muda mrefu kuuza bidhaa hizo sokoni .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents