FahamuHabari

Yaelezwa jimbo la Alabama nchini marekani, limepitisha muswada wa sheria kuwalazimu watu waliohusika na ubakaji kuondolewa nguvu za kiume

Yaelezwa jimbo la Alabama nchini marekani, limepitisha muswada wa sheria kuwalazimu watu waliohusika na ubakaji kuondolewa nguvu za kiume

Jimbo la Alabama nchini marekani limepitisha muswada wa sheria inayowalazimu baadhi ya watu waliopatikana na hatia ya kuwabaka watoto kupitia tiba ya kemikali itakayowaondolea uwezo wa kiume. Chini ya sheria hiyo, wale watakaopatikana na hatia ya kosa la kufanya tendo la ngono na watoto mwenye umri wa chini ya miaka 13 watalazimika kuanza kupata dawa za kuwapunguzia uwezo wa kufanya ngono mwezi mmoja kabla ya kuachiliwa kwa msamaha, Mahakama itaamua ni lini watakapokuwa hawahitaji tena dawa hiyo ya kikemikali.

Hadi sasa kuna majimbo saba , mkiwemo Louisiana na Florida, yenye sheria ya kumaliza nguvu za kiume kwa wanaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto wadogo.

Kwa mujibu wa BBC, Muswada wa sheria hiyo ulitiwa saini na Gavana wa jimbo la Alabama Kay Ivey Jumatatu. “Hii ni hatua kuelekea kuwalinda watoto katika jimbo la Alabama,” Alisema Bi Ivey.

Wenye hatia watatakiwa kulipia matibabu.

Hatua hiyo awali ilipendekezwa na Mbunge wa chama cha Republican Steve Hurst. Alisema amekuwa akiathirika sana kwa kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashirika yanayowalea watoto kuhusu namna watoto wadogo wanavyobakwa.

Mwaka 2009, wafungwa kadhaa nchini Uingereza walishiriki katika mradi wa uchunguzi wa dawa hizo ambapo walipoteza uwezo wao wa kufanya ngono kwa njia ya kemikaliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwaka 2009, wafungwa kadhaa nchini Uingereza walishiriki katika mradi wa uchunguzi wa dawa hizo ambapo walipoteza uwezo wao wa kufanya ngono kwa njia ya kemikali

Muswada huo umekosolewa na Muungano wa mashirika yanayopigania uhuru wa raia katika jimbo la Alabama. Mkurugenzi Mkuu wa Muungano huo Randall Marshall alikiambia kipindi cha told AL.com kuwa : “Haijawa wazi kwamba ni kweli zina athari yoyote na ikiwa imethibitishwa kimatibabu.

“Wakati jimbo linapoanzisha vipimo juu ya watu ,nadhani ni kinyume cha katiba .”

Kuondolewa uwezo wa kiume kwa njia ya kemikali ni nini?

Kwa matibabu ya kawaida mtu hupewa tembe au kwa njia ya sindano , ambavyo huzuwia uzalishwaji wa mbegu za uzazi za kiume na kuathiri uwezo wa mtu wa kuwa na hamu ya kufanya tendo la ngono.

Hata hivyo kwa kawaida mtu anaweza kurejeshewa uwezo huo wakati matibabu yanapositishwa.

Mwaka 2009, wafungwa kadhaa nchini Uingereza walishiriki katika mradi wa uchunguzi wa dawa hizo ambapo walipoteza uwezo wao wa kufanya ngono kwa njia ya kemikali.

Kwa matibabu ya kawaida mtu hupewa tembe au kwa njia ya sindano , ambavyo huzuwia uzalishwaji wa mbegu za uzazi za kiume na kuathiri uwezo wa hamu ya ngonoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKwa matibabu ya kawaida mtu hupewa tembe au kwa njia ya sindano , ambavyo huzuwia uzalishwaji wa mbegu za uzazi za kiume na kuathiri uwezo wa hamu ya ngono

Waliofanyiwa majaribio walikuwa ni wafungwa waliokuwa na “viwango vikubwa vya hamu ya ngono au matamanio makubwa ya kufanya tendo la ngono “.

Mwanasaikolojia wa Uhalifu Don Grubin alisema kuwa waliopewa dawa waliripoti kuwa na “mabadiliko katika maisha yao”.

Mwaka 2016, Indonesia ilipitisha sheria inayoidhinisha matumizi ya kemikali katika kuzuwia nguvu za kiume kama hukumu ya chini na kunhgongwa kwa wanaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto. Wakati huo , Prijo Sidipratomo kutoka Shirika la madaktari wa Indonesia alitaja mbinu hiyo kuwa v yenye “madhara” na iliyo “kinyume na haki za binadamu”.

Korea kusini ilipitisha sheria ya matumizi ya kemikali katika kuzuwia uwezo wa nguvu za kiume mwezi Julai, 2011.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents