Fahamu

Yaelezwa maafisa Kenya wafukua mwili ili kuuvua sare za kazi, Fahamu zaidi

Yaelezwa maafisa Kenya wafukua mwili ili kuuvua sare za kazi, Fahamu zaidi

Maafisa wa magharibi mwa Kenya wamefukua mwili wa mkaazi mmoja ili kumvua sare alizozikwa nazo kulingana na ripoti. Martin Shikuku Alukoye alizikwa akiwa na sare zake za huduma ya vijana wa kaunti ya kakamega baada ya kufa maji mwezi huu. Baadaye maafisa wa kaunti hiyo waliufukua mwili wake ili kumvua nguo hizo kulingana na ripoti.

Mjombaake bwana Alukoye alisema kwamba walikiuka sheria za nchi na tamaduni. ”Tuliishirikisha kamili serikali ya kaunti katika mipango ya mazishi na hawakupinga pendekezo letu kumzika akiwa na sare za kazini”, alisema Francis Mutamba.

Familia hiyo inasema kwamba ilipinga ombi kutoka kwa maafisa kuchukua nguo hizo kufuatia kuzikwa kwa jamaa huyo mwenye umri wa miaka 31, na kwamba mafisa waliamua kuufukua mwili huo bila idhini yao au agizo la mahakama. Naibu huyo wa chifu wa eneo la Ituti , Daniel Namayi alishutumu ufukuzi huo na kuonya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya maafisa hao.

”Mara tu mwili unapozikwa , utahitaji agizo la mahakama kwa mtu yeyote mwenye malalamishi kuufukua. Wasimamizi wa kaunti wameenda kinyume na sheria kwa kuufukua mwili swala ambalo ni kinyume na uatamaduni”.

”Tuliamua kumzika mwana wetu usiku kuambatana na tamaduni ambazo zinasema kwamba mtu aliyekufa maji hapaswi kuzikwa wakati kuna mwanga wa jua . Lakini maafisa wa kaunti wametushangaza wakati walipoamua kuufukua mwili ili kuchukua sare alizozikiwa nazo”, alisema bwana Mutamba. Mwili huo ulivishwa nguo mpya na kuzikwa tena mapema wiki hii baada ya wazee kufanya matambiko ya kuitakasa familia hiyo.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents