HabariTechnology

Yaelezwa mtandao wa facebook umelenga kuhakiki taarifa za Uongo, zinachapishwa kwa lugha za Kiafrika, sababu zaelezwa

Yaelezwa mtandao wa facebook umelenga kuhakiki taarifa za Uongo, zinachapishwa kwa lugha za Kiafrika, sababu zaelezwa

Mtandao wa kijamii wa Facebook, kwa ushirikiano na shirika la kuhakiki taarifa la Africa Check, umeanza mpango wa kufuatilia taarifa bandia zinazochapishwa katika mtandao huo kwa kutumia lugha za kiasili za kiafrika. Mpango huo uliozinduliwa mwaka jana katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika, sasa utajumuisha uhakiki wa lugha za Yoruba, Igbo, Swahili, Wolof, Afrikaans, Zulu, Setswana na Sotho.

KRAKOW, POLAND – 2018/12/05: Facebook logo is seen on an android mobile phone. (Photo by Omar Marques/SOPA Images/LightRocket via Getty Images)

Taarifa zitakazosadikiwa kuwa ghushi zitadhibitiwa hali ambayo itahakikisha haziwafikii watumiaji wengu wa mtandao huo ili zisisambazwe kwa urahisi.

Facebook inasema kuwa inategemea mrejesho kutoka kwa watumiaji wake kudhibiti taarifa bandia inapochambua uhalisia wa taarifa husika.

Mtandao huo wa kijamii wa umekuwa ukilamiwa vikali wa kusambaza taarika ghushi na kauli za uchochezi na chuki.

Facebook imekuwa ikilaumiwa kutodhibiti mitandao yao, sasa wajipanga kuchukua hatua

Barani Afrika pekee zaidi ya watu milioni 130 wanatumia mtandao wa Facebook.

Hivi karibuni Facebook iliunda mfumo mpya unaowalenga watu wanaoweka matangazo ya uongo kwenye mtandao huo.

Mfumo huo umekuja baada ya Martin Lewis, mwanzilishi wa tovuti ya Money Saving Expert, kushtakiwa baada ya jina na picha yake kutumika kwenye matangazo bandia kwenye ukurasa wa Facebook.

Facebook iliamua kuchangia kiasi cha pauni milioni 3 kwa ajili ya kutengeneza programu ya kupambana na wadanganyifu nchini Uingereza.

FacebookHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mtandao huo pia ulichapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019.

Katika kipindi hicho cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki – idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa.

Zaidi ya ujumbe milioni saba za”chuki” pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami.

Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina.

Mwanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg aliwakosoa baadhi ya watu wale wanaopendekeza kampuni hiyo ivunjiliwe mbali, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuka.

“Sidhani suluhisho ni kuvunjilia mbali kampuni kwasababu tunashughulikia [tatizo hilo],” Zuckerberg alisema.

Kwa sasa Taasisi ya kujitolea ya Citizens Advice imebuni laini ya simu ili iweze kuwasaidia watu wanapokutana na wadanganyifu mitandaoni-si tu kwa matangazo.

Citizens Advice imeainisha viashiria vitakavyojulisha kuwa matangazo ni bandia

  • Tangazo lisilo na uhalisia-au bidhaa iliyo na gharama ya chini kuliko inavyotarajiwa.
  • unapoambiwa ulipe haraka sana, au kwa njia isiyo ya kawaida-labda kwa huduma za kuhamisha fedha au kwa kutumia vocha.
  • Mtu kuwasiliana na wewe bila kutarajia.
  • kuulizwa kuhusu taarifa zako binafsi kama vile nywila (password) au pini.
  • tangazo lenye picha za watu maarufu .

Ndani ya Facebook, timu ya watu wenye ujuzi imeundwa kwa ajili ya kuchunguza matangazo yaliyoripotiwa kwa kutumia mfumo huu mpya.

Picha za simuHaki miliki ya pichaFACEBOOK

Kuanzia tarehe 16 mwezi Julai, watumiaji wa Facebook nchini Uingereza wameweza kubofya sehemu yenye madoa matatu kwenye ukingo wa kila tangazo, ili kuweza kuripoti matangazo wanayohisi ni ya udanganyifu.

Mamilioni ya watu wanajua kubaini matangazo bandia wakiyaona. Na mamilioni hawajui, hivyo wataalamu wanashauri kuyatambua kwa kutumia mfumo mpya wa kuripoti kwenye Facebook, na kuwalinda wale wasiojua.

Chanzo BBC.

By Ally juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents