Habari

Zitto Kabwe aivaa TAKUKURU, Adai wanavunja sheria na kutumika kisiasa

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kujisafisha kwanza yenyewe na kuepuka kutumika kisiasa.

Mhe. Zitto Kabwe

Mhe. Zitto amesema TAKUKURU ina miaka mitano haijakaguliwa na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na kila mwaka inapewa kiasi cha tsh bilioni 85 lakini mpaka sasa ni miaka mitano haijafunga hesabu wala kukaguliwa na CAG.

Zitto Kabwe amedai kuwa TAKUKURU kitendo cha kutokufunga hesabu za kila mwaka wanavunja kifungu chao wenyewe cha sheria namba 13 ya mwaka 2007 kifungu 47(2) kinachowataka kufunga hesabu za kila mwaka.

“TAKUKURU ni moja ya taasisi nyeti za uwajibikaji nchini Lakini inatumika kisiasa. Inatumwa na wanasiasa wa CCM kufanya mambo yao. Kukamatwa kwa Mwalimu Mukoba jana ni moja ya ushahidi wa kutumika kwa TAKUKURU kisiasa. Serikali Ina lengo ya kudhibiti Chama cha Walimu nchini na kina Mukoba walionekana ni vikwazo. Sitaki kusema la Nehemia Mchechu wa NHC Lakini nina hakika ya dhati amekuwa fixed sababu ya chuki, visasi na roho mbaya. TAKUKURU wanatumika kwenye hayo. Lakini Watanzania wajue kuwa TAKUKURU sio wasafi. Sheria yao inawataka wafunge hesabu kila mwaka na wakaguliwe na CAG. Licha ya kupewa tshs 84 bilioni kila mwaka, TAKUKURU hawana mahesabu ( annual accounts ) na hawajakaguliwa na mkaguzi yeyote. Jeshi letu JWTZ lina kaguliwa na CAG na kuitwa mbele ya PAC Lakini TAKUKURU hata hesabu hawafungi.”amesema Zitto Kabwe.

Kwa upande mwingine Zitto Kabwe ameitaka TAKUKURU kuacha kutumika kisiasa na kuionya kuwa isipokuwa makini huenda ikawa jumuiya ya nne la CCM.

“Nimepata kumwambia Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU uso kwa uso kuwa taasisi yake inatumika kisiasa. Narudia kumwambia hadharani kuwa taasisi yake inatumika. Wamejifanya wanamchunguza DC Mnyeti ambaye sasa ni RC hawajafanya na wala hawatafanya. Mimi simpendi Sadifa, Lakini najua Sadifa kakamatwa kisiasa tu. Watanzania tutoke tuiambie TAKUKURU iache kutumika kisiasa. Isafishe nyumba yake kwa kufunga vitabu vya hesabu na kukubali kukaguliwa na CAG. Iachie watu inaowakamata kwa siasa na ikamate watoa rushwa wa Kweli kama Mnyeti nk. Mlowola ajue kuwa TAKUKURU sio na haitakuwa Jumuiya ya 4 ya CCM baada ya Vijana, Wanawake na Wazazi. Kwa sasa tuwatake TAKUKURU kwanza wasafishe nyumba yao. Wanapewa tshs 84bn kila mwaka na Bunge. Sheria yao inawataka kila mwaka wafunge hesabu na zikaguliwe. Wana miaka 5 hawajafunga hesabu wala hawajakaguliwa na CAG. Nashangaa sana donor countries zinazowapa fedha bila ukaguzi.”amesema Zitto Kabwe.

Soma taarifa yake kamili aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Facebook.

TAKUKURU ni moja ya taasisi nyeti za uwajibikaji nchini Lakini inatumika kisiasa. Inatumwa na wanasiasa wa CCM kufanya mambo yao. Kukamatwa kwa Mwalimu Mukoba jana ni moja ya ushahidi wa kutumika kwa TAKUKURU kisiasa. Serikali Ina lengo ya kudhibiti Chama cha Walimu nchini na kina Mukoba walionekana ni vikwazo. Sitaki kusema la Nehemia Mchechu wa NHC Lakini nina hakika ya dhati amekuwa fixed sababu ya chuki, visasi na roho mbaya. TAKUKURU wanatumika kwenye hayo.

Lakini Watanzania wajue kuwa TAKUKURU sio wasafi. Sheria yao inawataka wafunge hesabu kila mwaka na wakaguliwe na CAG. Licha ya kupewa tshs 84 bilioni kila mwaka, TAKUKURU hawana mahesabu ( annual accounts ) na hawajakaguliwa na mkaguzi yeyote. Jeshi letu JWTZ lina kaguliwa na CAG na kuitwa mbele ya PAC Lakini TAKUKURU hata hesabu hawafungi.

Nimepata kumwambia Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU uso kwa uso kuwa taasisi yake inatumika kisiasa. Narudia kumwambia hadharani kuwa taasisi yake inatumika. Wamejifanya wanamchunguza DC Mnyeti ambaye sasa ni RC hawajafanya na wala hawatafanya. Mimi simpendi Sadifa, Lakini najua Sadifa kakamatwa kisiasa tu.

Watanzania tutoke tuiambie TAKUKURU iache kutumika kisiasa. Isafishe nyumba yake kwa kufunga vitabu vya hesabu na kukubali kukaguliwa na CAG. Iachie watu inaowakamata kwa siasa na ikamate watoa rushwa wa Kweli kama Mnyeti nk. Mlowola ajue kuwa TAKUKURU sio na haitakuwa Jumuiya ya 4 ya CCM baada ya Vijana, Wanawake na Wazazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents