Burudani
Hanscana: Nipo tayari nimlipe mtu ili anikutanishe na Godfather
Mtayarishaji wa video anayefanya vizuri na mshindi wa Tuzo za Watu, Hanscana amesema yupo tayari amlipe mtu ili amuunganishe na muongozaji mkongwe wa video wa Afrika Kusini, Godfather.
Hanscana ameiambia Bongo5 kuwa akikutana na Godfather atajifunza vitu vingi.
“Godfather ni mtu mkubwa sana,” amesema Hanscana.
“Unajua mimi kwake ni kama naanza kazi, natamani sana kukutana naye. Nipo tayari nimlipe mtu ili anikutanishe na Godfather. Ana experience kubwa na kazi hii, kwahiyo kwangu ni mtu muhimu sana.”