Habari
Polisi wahimizwa kuhakikisha usalama kwa wananchi
Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, amelitaka jeshi la polisi nchini kuhakikisha wananchi wanaishi katika hali ya usalama.
Ameyasema hayo katika ziara yake mkoani Shinyanga wakati akikagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na magereza, vikosi vya polisi,uhamiaji,vikosi vya zima moto na uokoaji.
“Jeshi la polisi linaposhindwa kuwajibika katika suala zima la usimamizi wa ulinzi na usalama wa raia, ipo hatari ya kuongezeka kwa matukio ya jinai kwenye maeneo mengi ya nchi na kusababisha hofu kwa wananchi,” alisema.
Aidha Nchemba alisema jeshi la polisi duniani kote kazi yake ni kuhakikisha wananchi wanakuwa katika hali ya usalama na utulivu muda wote.
BY: EMMY MWAIPOPO