Dar Mpya ya Makonda: Makonda afanya ziara jijini Dar kusikiliza kero za wananchi
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akitoa maagizo kwa baadhi ya viongozi
Ziara hiyo imeanzia katika wilaya ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda kusikiliza kero za wananchi mtaani, Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
Akiongea na viongozi hao wa wilaya ya Kigamboni, Makonda amesema anafanya ziara hiyo ili kugundua kero za wanachi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa serikali kuwajibika.
“Nataka wafanyakazi wafanyekazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wetu, nimegundua 80% ya wafanyakazi wa serikali hawafanyikazi, asilimia 80 ya watumishi wa umma hawafanyikazi, niwapiga majungu, wasoma magazeti, niwambea. Kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara,” alisema Mkonda.
Pia Makonda alisema hataki kuona wananchi wanakimbilia kwa mkuu wa mkoa kuomba msaada wa utatuzi wa changamoto zao wakati serikali ina wafanyakazi kuanzia ngazi ya vitongoji.
Aidha mkuu huyo ataelekea mtaa wa Maweni, Mjimwema ambapo ataangalia uharibifu wa mazingira uliosababishwa na wachimba kokoto.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Paul Makonda
Viongozi na watumishi wa idara mbalimbali za Wilaya ya Kigamboni
Mkuu wa Wilaya na Kinondoni Ally Hapi