Michezo
Sevilla yatinga fainali ya Copa del Rey kibabe
Klabu ya Sevilla usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kutinga fainali ya kombe la Mfalme nchini Hispania kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Leganes.
Kwenye mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1 ambapo Sevilla imetinga fainali kwa jumla ya magoli 3-1.
Magoli hayo yaliyofungwa na Joaquin Correa na Franco Vazquez yamekamilisha safari ya Secvilla ambapo leo kuna mtanange mwingine kati ya Barcelona na Valencia ili kupata timu nyingine ya kwenda fainali.