Burudani
“Bongo Movie haijafa bali imevamiwa na watu wasio na elimu, utamuuzia nani filamu iliyoandaliwa kwa mil. 1” (+video)
Mchekeshaji na Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Idrisa Makupa amewajia juu watu wanaosema kuwa tasnia ya filamu nchini imekufa.
Akiongea na Bongo5, Makupa amesema kuwa tasnia hiyo haijafa bali hapa katikati imeingiliwa na watu wasiokuwa na taaluma hiyo ambao wamepelekea utengenezwaji mbovu wa filamu uliopelekea soko kuyumba.
Akielezea gharama za utengenezaji wa filamu zenye ubora amesema filamu nzuri ya kiwango cha kawaida lazima angalau uwe na milioni 15 hadi 20 lakini kuna wahuni wanatumia milioni 1.