Burudani

Taarifa rasmi: Kinachoendelea kuhusu msiba wa mtoto wa Muna ‘Patrick’ na ratiba

Mtoto Partick wa mwanadada mjasiriamali, Muna na Casto Dickson amefariki usiku wa jana baada ya kuwa kwenye koma kwa muda wa wiki moja.

Mtoto huyo alipelekwa Kenya wiki iliyopita kwaajili ya kufanyiwa upasuaji ambao haukuelezwa ni upasuaji wa nini lakini mtoto huyo alikuwa anasumbuliwa na mguu kwa muda mrefu.

Mapema jana mkurugenzi wa vipindi Wasafi TV, Zamaradi Mketema ambaye alipewa jukumu na familia la kuzungumza, jana alianza alianza arakati za kukusanya michango kwaajili ya matibabu ya mtoto huyo.

Leo, Zamaradi ametoa taarifa hii rasmi kuhusu msiba huo.

Kwasasa bado Mwili uko Nairobi (Kenya) na wameshaanza taratibu nyingine ili kufanikisha mwili kufika hapa nchini.

Na kama kila kitu kikikamilika mwili unatarajiwa kuletwa siku ya keshokutwa hapa DSM na ndio taratibu nyingine zitafata

Ila kwasasa makutano yatakuwa Mbezi Beach kwa Muna kwa wale ndugu jamaa na marafiki watakaotaka kujumuika na zaidi tu michango bado inahitajika sana sana ili kuweza kukamilisha taratibu zilizopo kama mnavyojua lazima kuna mambo ya hospitali yaliyokuwepo, taratibu za kusafirisha na mengineyo (namna ya kutuma nimetoa maelekezo kwenye post iliyopita ambayo itamfikia yeye mwenyewe)

Ushirikiano ni muhimu zaidi kwa kipindi hiki bila kusahau MAOMBI juu ya mwenzetu alieondokewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents