Michezo

Kwa Kibu Simba wasiangalie Takwimu – Edo Kumwembe

“Takwimu zinatuonyesha Kevin De Bruyne ni bora kuliko Zinedine Zidane. Macho yetu yanatuambia Zidane ni bora kwa mbali kuliko staa huyu wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji. Takwimu zinatuonyesha Cristiano Ronaldo ni bora kuliko Diego Maradona na Ronaldo De Lima. Hali halisi inatuambia hao wawili ni bora kuliko Ronaldo. Hapa ndipo linapoibuka suala la Kibu.

Hana mabao mengi lakini kuna kitu ambacho Simba wanakiona kwa Kibu kuliko kwa wachezaji wengine. Ukiwaambia Simba nani aondoke kati ya Kibu au Freddy Michael watakwambia Freddy aondoke ingawa ni huyu huyu amefunga mabao mengi kuliko Kibu. Soka la namba linatuchanganya katika dunia ya kisasa. Unajaribu kushindana na hali halisi. Hapa ndipo Kibu anapohitaji pesa nyingi katika mkataba wake. Hapo ndipo Kibu anadengua.” — Edo Kumwembe.

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents