Habari

Wadau waombwa kushirikiana na serikali kukabiliana na utapiamlo

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ametoa rai kwa wadau wa sekta binafsi kushirikiana serikali katika kukabiliana na swala la utapiamlo nchini.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 24/05/2024 Jijini Dar e Salaam wakati kikao kilichohusisha wadau wa sekta binafsi katika kujadili maandalizi ya Mkutano wa 10 wa lishe unaotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza Mwezi Septemba.

Katika biashara tunahitaji watu ambao wanaoweza kufikiri haraka katika hatua za ukuaji wa kiuchumi, ili fikra hizo ziendelee tunahitaji kujenga Jamii bora.

“Lazima tuunganishe nguvu tukabiliane na changamoto ya udumavu katika Jamii yetu ili kampuni zetu za ndani ziweze kuendelea katika ushindani na kampuni za nje,” alihimiza

Aidha sekta binafsi imepata nafasi ya kutambulika na kushikana mkono na serikali ili kuwa na juhudi za pamoja katika kuhakikisha taifa letu linakabiliana na tatizo la lishe nchini kwa uendelevu mkubwa.

“Tunahitaji kuwa na taifa lenye watu wenye afya nzuri, siha njema wanaoweza kufikiri, wanaoweza kuweka mikakati na kuongeza ushawishi wa kibiashara nje ya mipaka ya nchi yetu,” alisema.

Kwa upanda wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna amesema sekta binafsi wanayo nafasi ya kuhamasisha walaji katika kujenga hamasa ya kuleta mabadiliko chanya katika lishe kulingana na bidhaa zinazozalishwa.

“Tatizo la utapiamlo lisipopatiwa ufumbuzi, linaweza likapunguza nguvu ya ununuaji (Purchasing Power) hata kama bidhaa zitakuwa bora na muhimu,”Alibainisha.

Naye Ally Sechonge kutoka kampuni ya Tanga Freshi amesema kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya maziwa ni 4% ya Maziwa yanayotoka kwa Ng’ombe ndio yanayosindikwa na 96% yananywewa bila kusindika.

“Tatizo kubwa ni kwamba walaji wanakuwa na maamuzi jinsi gani watatumia fedha yao, bila kuzingatia swala la utaratibu mzuri wa kula,” alisema.

Naye Iddi Mvungi kutoka kutoka kampuni ya Bakhresa ameishukuru serikali kwa kujumuisha sekta binafsi katika mapambano dhidi ya utapiamlo.

Sisi tunaendelea kuihakikisha serikali kwamba tutakuwa pamoja na Serikali na kwa kuhakikisha maelekezo yote yanayoelekweza, tunayazingatia katika uzalishaji wa bidhaa.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents