Michezo

Eng. Hersi awa Gumzo Afrika

SAFARI YA INJINIA, LUBUMBASHI . Yanga imeanza kwa kasi mbio za usajili na safari hii haitaki kuambiwa, inapanda mwewe kujionea yenyewe ubora wa mastaa inaowataka, yaani kisasa zaidi na unavyosoma hili Rais wa klabu hiyo, Hersi Said yupo jijini Lubumbashi, DR Congo  akiwafuata mastaa wawili wapya.

Tuanze na juzi. Hersi alikuwa Uwanja wa Kibasa Maliba akitazama mchezo wa Ligi Kuu ya DR Congo Lubumbashi Sport dhidi ya TP Mazembe uliomalizika kwa suluhu. Kwenye mchezo huo Lubumbashi Sport anayoichezea beki wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ikicheza soka la kujilinda ikainyima ushindi Mazembe na baada ya mchezo huo Hersi alifanya kikao kifupi na Ninja akitaka kufahamu maendeleo yake lakini ziara yake ikaendelea na jana akitua kwenye mchezo mwingine mgumu.

Jana Hersi akatua Uwanja wa Victoria kutazama mechi nyingine ya Ligi Kuu nchini humo kati ya AS Union Maniema dhidi ya FC Lupopo lakini Arena tunafahamu kigogo huyo aliyeibadili Yanga kwa hesabu kali za usajili aliwafuata mastaa wawili kutoka kwenye timu zote hizo.

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents