Habari

Msaada unahitajika Magara maji yaliyofurika ziwa Manyara

Mwenyekiti wa Kijiji cha Manyara kata ya Magara wilaya ya Babati mkoani Manyara Juma Jokoda, amesema bado wanahitaji msaada baada ya makazi yao kuvamiwa na maji yaliyofurika Ziwa Manyara.

 

Amesema msaada mkubwa unaohitajika kwa haraka ni mahema kwa ajili ya kuwapatia hifadhi na chakula.

Jokoda amesema kitongoji cha Kambi ya fisi kimeathiriwa zaidi na maji hayo na kwamba Wanafunzi wanashindwa kuvuka kwenda shuleni.

Amesema mpaka sasa msaada walioupata ni wa chakula gunia kumi za mahindi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Daniel Sillo.

Maji hayo yaliyovamia makazi ya watu tangu April 26,2024 yamesababisha kaya zaidi ya 140 kukosa pa kuishi.

Mvua kubwa zilizonyesha hadi mwezi april mwaka huu zimesababisha Ziwa Manyara kujaa kufuatia mito inayotiririsha maji kutoka Mbulu, Monduli na Babati.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents