Habari

Watu 18 Wajeruhiwa, Ajali ya Basi Singida

Basi la kampuni ya Takbir lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Katoro mkoani Geita limepata ajali leo Mei 23, 2024 saa moja asubuhi katika eneo la Manga mkoani Singida na kujeruhi watu 18.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP. Amon Kakwale amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa ajili ya matibabu.

Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa basi hilo limepata ajali baada ya kuyumba mara kadhaa na kugonga kingo za barabara na kisha kupinduka wakati likijaribu kulikwepa gari dogo lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents