Michezo

Lameck Lawi kuvaa viatu vya Inonga

Unaweza kusema ndani ya Simba eneo la beki wa kati mwenye namba yake yupo njiani kutua kikosini hapo baada ya klabu hiyo kufikia dau linalotakiwa na Coastal Union kwa ajili ya kumuachia Lameck Lawi (18).

Lawi amekuwa akiwindwa na Simba kutokana na uwepo wa taarifa za beki wa kati wa timu hiyo, Henock Inonga kuwa njiani kuondoka baada ya kuwepo kwa ofa mezani. Inonga anatajwa kutakiwa na FAR Rabat ya Morocco.

Uongozi wa Coastal ulisisitiza kuwa bila ya Sh 200 milioni, beki huyo mwenye umri wa miaka 18 hataenda popote na badala yake atabaki klabuni hapo kumalizia mkataba wa miaka miwili uliosalia. Simba imekubali kulipa kile ambacho timu inayommiliki mchezaji huyo inakitaka ili ipate huduma yake msimu ujao.

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

cc: Sports Arena

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents