Habari
Rais Magufuli “Nampenda Kangi Lugola lakini kwenye hii nafasi hapana” – Video
''Lugola ni mwanafunzi wangu, nimemfundisha pale Sengerema Sekondari, pamoja na ukubwa wake lakini kwenye hili hapana''
Rais wa Jamhuri ya muugano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli leo katika uzinduzi wa makazi ya Askari Magereza Ukonga Dar es salaam amesema kuwa Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Kangi lugola pamoja na katibu mkuu wake Meja Jenerali Jacob Kingu amemuandikia barua ya kujiuzulu na amemkubalia.
”Hivi karibuni kulikuwa na mkataba wa ajabu unatengenezwa na wizara ya mambo ya ndani wenye thamani ya Euro millioni 408,mradi ambao umetayarishwa na kusainiwa na kamishna Jenerali Kingu ambao haujapitishwa na bunge”.
”Yanayokwenda kununuliwa kwenye mkataba ni ya hovyo cjui madrone cjui ma nini ni ya ajabu,mimi nitaendelea kuwapenda ila kwenye hii position hapana,”amesema Rais Magufuli.
Na Jacquiline Ngoya.