Burudani

Achana na Awilo Longomba wa Atittude ya Harmonize, huyu ndiye halisi (Video)

PART 1: WATOTO WA 2000 TULIENI KWANZA HII SIO AMAPIANO 😂

#oldisgold: Jina lake halisi ni Louis Albert William Longomba alimaarufu kama Awilo Longomba, alizaliwa May 5, 1962 Katika jiji la Kinshasa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo zamani likijulikana kama Léopoldville.

Alifanikiwa kutoa album kadhaa zikiwemo:

1. Moto Pamba (1995)
2. Coupe Bibamba (1999)
3. Kafou Kafou (2001)
4. Mondongo (2003)
5. Super-Man (2008)

Lakini pia alifanikiwa kufanya nyimbo nyingi sana na miongoni mwa ngoma zake maarufu ni kama:-

1 Coupé Bibamba” (featuring Jocelyne Béroard)
2. Karolina”
3. Champion”
4. Mondongo”
5. Fidele”
6. Gate li coin.

Alifanya muziki wa Techno-soukous!na ndombolo.

Moja ya tukio maarufu zaidi lisiloweza kusahaulika katika maisha yake ya muziki ni pale alipofanikiwa kuujaza Uwanja wa Mpira wa Lagos Nigeria kwa kufanya Show siku tatu mfululizo Uwanja wa Lagos ukiwa FULL HOUSE wenye uwezo wa kuingiza watu 55,000 mwaka 2000 na rekodi hii haijawahi kuvunjwa hata na msanii kutoka Nigeria.

Awilo alifanikiwa kufanya Tour karibu maeneo mengi ya dunia hasa Ulaya na Marekani, alisifika kwa staili yake ya kucheza.

Ilikuwa ngumu sana uende kwenye harusi au Sherehe miaka hiyo usisikie Wimbo wowote wa Awilo Longomba, ugomvi ungetokea.

Alianza kufanya muziki miaka ya 1980, Baba yake alikuwa mwanzilishi wa kundi la OK Jazz mwaka 1956 na lilikufa mwaka 1993.

Tutafutieni Mkongo mmoja atuambie GATE LI COIN maana yake nini?? 😂😂

Ngoma za Awilo Longomba zinakukumbusha wapi na lini??

 

https://www.instagram.com/reel/C8K3NU0tV8z/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents